Kifua Kikuu (TB) ni miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani na Umoja wa Mataifa (UN) umeripoti kuwa TB inaua watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wowote wa kuambukiza
Dalili zake ni pamoja na kikohozi cha muda mrefu, kukosa hamu ya kula, kukohoa damu, homa, kutokwa jasho usiku, kupungua uzito na uchovu
TB ni ugonjwa unaotibika lakini wengi huacha kutumia dawa kabla ya muda waliopangiwa na hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa kuugua kwa muda mrefu zaidi .
March 24 ya kila mwaka tunaadhimisha siku ya kifua kikuu duniani.
Kwa mwaka huu shirika la mwitikio wa kudhibiti kifua kikuu na ukimwi tanzania {MKUTA} limetumia siku hii kuibua wagonjwa kweny wilaya mbalimbali walio wapya na waliokatisha dozi zao na kuwapatia elimu pamoja na matibabu ilikufikia adhma ya serikali kutokomeza TB ifikapo 2035.