Jeshi la Polisi Nchini leo Machi 24, 2024 limemuaga rasmi Kamishna Mstaafu wa Polisi Nsato Marijani baada ya kustaafu Utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Akiongea mara baada ya Sherehe hizo Kamishna Mstaafu Marijani amewata Askari Polisi wanaoendelea na Utumishi wao kudumisha nidhamu pamoja na kuendelea kuongeza maarifa ili kwendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo amebainisha kuwa mbinu zinabadilika kila siku kutokana na maendeleo ya sayansi.
Naye Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ameelezea hatua mbalimbali alizopitia Kamishna huyo Mstaafu.
Sherehe hizo ambazo zimefanyika Shule ya Polisi Tanzania- Moshi zilihusisha gwaride maalumu ambalo alilikagua na baadaye kupanda gari maalumu lililosukumwa na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi.