Wahamiaji haramu 20 raia wa Ethiopia wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara pamoja na Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma kwa makosa ya kusafirisha Wahamiaji hao kinyume cha sheria.
Akiongea na Ayo Tv Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 Mwaka huu ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na wahamiaji haramu ishirini raia wa Ethiopia kwa kutumia gari namba T.774 BDL Land Cruiser huku ikiwa na bendera ya Chama Cha Mapinduzi CCM
“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na watanzania ilibidi tuweke gari Pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji haramu 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha,Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji” kaimu RPC Manyara