Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameishutumu Israel kwa “kusababisha kiu kimakusudi” na kueneza magonjwa huko Gaza, kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina, WAFA.
Abbas aliyasema hayo katika Siku ya Maji Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 22.
“Siku ya Maji Duniani mwaka huu inakuja wakati ambapo watu wetu wa Palestina huko Gaza wanakumbwa na uhalifu wa kikatili wa uvamizi huo, ambao umegharimu maisha ya maelfu ya wahanga wasio na hatia, wakiwemo mashahidi, waliojeruhiwa, wengi wao wakiwa watoto. wanawake, na wazee,” alisema.