Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki na kuhutubia katika Mkutano wa tatu wa Mtandao wa Wabunge wasiofungamana na upande wowote uliofunguliwa na Spika wa Bunge la Azerbaijan, Mhe. Prof. Sahiba Gafarova, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya President Wilson Geneva, nchini Uswisi Leo tarehe 25 Machi, 2024.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amempongeza Mwenyekiti wa Mtandao huo Prof. Sahiba kwa Uongozi wake mzuri uliofanikisha hatua kubwa ya kupambana na athari za Mabadiliko ya tabianchi duniani tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022.