Nakumbuka kwenye bunge la bajeti Tanzania lililoisha hivi karibuni kuna stori ziliongelewa za Mchina ambae alijinyonga Morogoro baada ya kugundua kwamba kazi ya ujenzi aliyoifanya haikuwa kwenye kiwango kinachotakiwa.
Leo kwenye hii post anahusika raia mwingine wa Asia lakini huyu ni kutoka Japan, Mwanasiasa huyu maarufu aitwae Ryutaro Nonomura amekua kwenye headlines za tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zikiwemo safari nyingi alizozifanya kutembelea maeneo mbalimbali.
Kilio hiki cha kupinga tuhuma alikiangua kwenye mkutano na Waandishi wa habari baada ya kuulizwa kuhusu matumizi mabaya ya hizo fedha ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 40 za Kitanzania baada ya wiki iliyopita kukosolewa.
https://www.youtube.com/watch?v=Rhw6nvP3MEI
Ni mwanasiasa gani wa Tanzania anakuvutia kwenye utendaji kazi wake?
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB