Nchini Sudan Kusini, vyama vya upinzani vinapinga ongezeko kubwa la ada wanayotakiwa kulipia ili kujisajiliwa kama wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka huu ambapo sasa watalazimika kilipa dola za Marekani elfu 50.
Hatua hii inakuja wakati ambapo raia wa Sudan Kusini wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwezi Desemba mwaka huu, uchaguzi ambao tayari upinzani unahoji kiwango cha tozo ya kuchukua fomu za kugombea.
Tangazo la kuvitaka vyama vya siasa kulipa Dolla elfu 50 kushiriki uchaguzi huo lilitolewa na kamati iliyopewa jukumu la kuratibu uchaguzi huo.
Awali vyama vya siasa vilitakiwa kulipia ada ya Dolla 150 huku kamati inayoratibu maandalizi ya uchaguzi huo ikikosa kutoa sababu za kuongeza ada.