Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) imesema ina imani kubwa na maono ya serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kufanya sekta binafsi inaendelea kukuwa kwa kasi na kuwa shindani nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Raphael Maganga wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya Sekta binafsi kuhusu Dira ya maendeleo ya Tanzania mwaka 2050
“Tunashukuru serikali kupitia wizara ya mipango kwa kuendelea kujenga imani kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na tungependa pia kuona Dira ya 2050 ikilenga kuweka kwa mazingira mazuri zaidi juu ya masuala ya utawala bora na utawala wa sheria kataka kukuza sekta binafsi kwa maendeleo ya taifa.”Amesema Maganga.
Maganga ameongeza kuwa mkutano huo unatoa fursa ya kusikiliza mijdala ya wajumbe wa mkutano huo kusikiliza tathimini kutoka Tume ya mipango kuhusu utekelezaji wa Dira ya maendeleo ya maendeleo ya 2025, changamoto na hatua muhimu zilizofikiwa katika uaandaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa (TDV) 2050 ili kuimarisha ushirikiano na Ushirikishwaji wa wadau.
“Lazima tujenge Tanzania ijayotegemea ufumbuzi na Teknolojia ikiwemo kuwekeza katika tafiti za hali ya juu ili kuwezesha nchi kufikia viwango vipya vya ufanisi na ushindani wa kimataifa katika biashara.”Amesisitiza Maganga
Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi huyo amesema TPSF inajitahidi kuweka mazingira ya uwazi na uwajibikaji na rafiki ya uwekezaji yakisimamiwa na mfumo thabiti wa kisheria unaowezesha sekta binafsi kustawi na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye ustawi wa taifa.
“Katika kutekeleza majukumu yake,TPSF imekuwa mstari wa mbele wa kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na baishara nchini yanahimarika,kwa kuwa na kanuni,sera na sheria hivyo kupunguza umaskini nchini.”Ameongeza Maganga
Wadau mbalimbali kutoka sekta ya usafirishaji kwa njia maji na nchi kavu pamoja na wadau wengine wa maendeleo ya Jamii kutoka sekta ya Umma wamehudhuria mkutano huo.