Baada ya upekuzi uliofanyika katika nyumba za Sean ‘Diddy’ Combs al maarufu kama P Diddy, Wakili wake alikashifu mamlaka ya serikali kwa kutumia “kiwango kikubwa cha kijeshi” wakati wa kuvamia nyumba za rapa huyo katika jimbo la Florida na California mwanzoni mwa wiki hii.
Nguli huyo wa muziki wa hip hop kwa sasa anachunguzwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono pamoja na kufanya biashara za ngono kulingana na vyanzo vya sheria, madai ambayo wakili wake, Aaron Dyer, amekosoa upekuzi uliofanyika na kuuita “witch hunt” akimaanisha ni kama wanajaribu kumfichua na kumtafuta mwanga au mchawi aliyejificha, akiongeza kuwa jana kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu za kijeshi wakati upekuzi huo ukifanyika katika makazi ya P Diddy.
Kulingana na maelezo ya wakili wa PDiddy kwa TMZ, Mamlaka ya usalama walitumia nguvu kubwa pamoja na kuonyesha hali ya uadui kutokana na jinsi watoto wa rapper huyo pamoja na wafanyakazi wake walichofanyiwa.
Watoto wa P Diddy Justin Combs (30) na Christian King Combs (25) walitiwa mbaroni kwa muda mfupi na kuzuiliwa baada ya kuondolewa kwenye nyumba yao iliyopo Beverly hills jijini Los Angeles California, lakini hawakufanya kuwa sehemu ya uchunguzi wa mamlaka.
Mamlaka ililenga makazi mawili ya P Diddy (54) jijini Los Angeles pamoja na Miami na kulingana na taarifa kutoka vyanzo cya sheria, kwenye msako huo mamlaka ilichukua simu pamoja na computer zake, wakiacha nyumba hizo zikiwa hazitamaniki yani vitu vilitupwa tupwa, na kupanguliwa panguliwa.
Kulingana na taarifa kutoka kwa mwanasheria wake, P Diddy, hakukamatwa au kushtakiwa lakini alizungumza na kushirikiana na mamlaka na Usafiri wake haujazuiliwa kwa njia yoyote, aliongeza.