Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia yuko katika klabu ya Aston Villa kwa msimu mzima akitokea Galatasaray, ambako ana mkataba hadi 2027, na amepata ugumu kuzoea ugenini.
“Ninaikosa Italia sana,” fowadi huyo wa zamani wa Roma alisema. “Ninakumbuka familia yangu, marafiki zangu, mwanangu. Lakini ni juu ya klabu yangu, Galatasaray, kuzingatia mustakabali wangu.”
Alipoulizwa kuhusu kuhamia AC Milan, aliongeza: “Nani anajua. Nimemwambia tu wakala wangu, Claudio Vigorelli, anifahamishe kunapokuwa na kitu thabiti. Kwa sasa lazima niangazie Aston Villa.”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameichezea Villa mechi 20 za ligi, ingawa ni mechi saba tu kati ya hizo ndio ameanza.
“Nimecheza chini ya ilivyotarajiwa katika Ligi Kuu,” alisema. “Nilipofika Uingereza sikuzungumza hata lugha. Ni vigumu kutulia, pia kwa sababu wachezaji wenzangu wengi wameoa na nimetumia muda mwingi peke yangu.”