Ikijiandaa kwa uvamizi wa Rafah, Israeli inaagiza mahema 40,000 kutoka nchini China.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameagiza ununuzi huo ili kuwekwa katika eneo lililozingirwa la Gaza, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti, ili kujiandaa na uvamizi wa ardhini katika mji wa Rafah ambapo zaidi ya Wapalestina milioni 1.5 waliokimbia makazi yao wamekimbilia hifadhi.
Inakuja wakati Netanyahu akipuuzilia mbali hofu ya kimataifa ya janga la kibinadamu ikiwa Israel itaanzisha uvamizi wa ardhini uliopangwa katika mji wa kusini mwa Gaza, akisema raia wataweza kuyakimbia mapigano katika maeneo mengine ya eneo lenye vita.