Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaita wawekezaji wa Kimataifa kuja nchini, kutokana na mazingira bora zaidi yanayovutia uwekezaji na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji ikiwemo sera, utulivu, maliasili na eneo la kijiografia.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ametoa wito huo wakati akifunga kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ameyataja baadhi ya maeneo yenye fursa za uwekezaji ikiwemo afya, elimu na miundombinu na kwamba Serikali ya a Jumhuri ya Muungano wa Tanzania nchini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira wezeshi.
Kongamano hilo ambalo pia limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali nchini, limejumuisha zaidi ya makampuni mia mbili, sitini yakiwa ni kutoka Mkoa wa Zhejiang nchini China, arobaini yakiwa ni makampuni ya China yaliyowekeza nchini, na makampuni zaidi ya mia moja yakiwa ni kutoka Tanzania.
Kuhusu uwekezaji, Mhe. Mpango ameyasifu makampuni na wafanyabiashara kutoka China kwa kuendelea shiriki maendeleo ya uchumi nchini kupitia uwekezaji wao huku akitoa takwimu mbalimbali za kuongezeka kwa mapato na uchumi ikiwemo Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi Desemba 2023, ambapo kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kilisajili zaidi ya makampuni 256 kutoka China, yakiwa na uwekezaji wa takribani Dola Bilioni 4 za kimarekani.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema uukiifuatilia historia ya ushirikiano kati ya Tanzania na China pamoja na uhusiano wa kidiplomasia ambao leo unatimiza miaka 60, hivyo wao Wachina na Watanzania ni ndugu.
Amesema kuwa maendeleo makubwa ya utulivu pamoja na uongozi madhubuti wa Serikali, wafanyabiashara wengi wa China wamevutiwa kuja kuwekeza Tanzania, na zaidi mapokezi wanayopata yanawafanya waendelee kushiriki
Pia amesema Tanzania ni kiungo muhimu katika ushirikiano kati ya Afrika na China, na hivi Karibuni, Rais Xi Jinping aliweka bayana kuwa Uhusiano wa China na Tanzania ni ushirikiano namba moja kwa viwango ikilinganishwa na mahusiano mengine ya nchi mbili kati ya China na nchi za Afrika.
“Tuna matarajio makubwa ya Maendeleo ya ushirikiano wa Tanzania na China, ambao misingi yake imejengwa kwenye historia, ujenzi wa ushirikiano wa kiuchumi unaoendelea na urafiki wa kuamainia.”
Awali Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wa serikali ya Jinhua nchini China Zhu Chonglie amesema wao kama Mkoa wa Zhejiang, na Serikali yetu ya Jiji la Jinhua kama ilivyo katika maeneo mengine ya China na Tanzania tunashiriki kuadhimisha mafanikio yaliyopatikana katika miaka 60, mfano mzuri ni Kongamano kubwa la elimu liliratibiwa na chuo chetu cha Zhejiang (Zhejiang Normal University Tanzania China Education Forum).
Elimu ni Moja ya maeneo yalitusaidia pamoja kuimarisha uhusiano Wetu wa kihistoria ambao tunapaswa kuuendeleza, na ndio maana chuo chetu cha Zhejiang kimewekeza zaidi kwenye mabadilishano ya kielimu na vyuo mbalimbali vya elimu barani Afrika, ikiwemo Tanzania na mfano mzuri ni katika Chuo Kikuu cha Dsm, kupitia ujenzi wa Taasisi ya Confucius na maktaba Kuu.
Kwenye upande wa Utamaduni pia, Jiji letu na Mkoa mzima wa Zhejiang, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika kupokea vikundi mbalimbali vya maonyesho ya Utamaduni lakini pia Vikundi mbalimbali vya Tanzania vimefika Zhejiang kubadilishana uzoefu.
Hata ujio Wetu hapa kwa ajili ya Kongamano hili la Uwekezaji ni matokeo ya ushirikiano wa kihistoria uliopo lakini na ukuaji unaoendelea, tunapaswa kuutunza kupitia mabadilishano kama haya ya kiuchumi, watu na watu pamoja na kubadilishana uzoefu wa masuala la kisiasa.