Magari matatu ambayo ni Mabasi mawili ya New Force na Sauli na lori moja, yamepata ajali na kuteketea kwa moto leo March 28 2024 Mlandizi Mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge tayari amefika eneo la tukio akiwa na RPC Pwani na muda sio mrefu ataongea na @AyoTV_ na kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hili.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishirikiana na Jeshi la Polisi na Taasisi nyingine wameendelea kuzima moto