Vikosi vya Somalia viliwaua takriban wanamgambo 80 wa al-shabaab, wakiwemo baadhi ya viongozi wa kundi hilo, katika operesheni za kijeshi zilizoendeshwa kwa msaada wa washirika wa kimataifa, shirika la habari la serikali lilisema.
Operesheni hizo zilifanyika Galmudug, Hirshabelle na Jimbo la Kusini-Magharibi kwa muda wa siku mbili zilizopita.
Inakuja siku chache baada ya kundi la kigaidi lenye mafungamano na al-Qaeda kushambulia kambi ya kijeshi katika eneo la Lower Shabelle.
Wapiganaji wake walipigana kuelekea kwenye kituo hicho kwa kutumia mabomu ya kujitoa mhanga kwenye gari. Wanajeshi saba wa Somalia, akiwemo kamanda wa kambi hiyo, na wapiganaji 10 wa al-Shabaab waliuawa katika mapigano hayo.
Kundi hilo limekuwa likipigana kwa takriban miongo miwili, likilenga kuiangusha serikali kuu ya Somalia.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitangaza Desemba mwaka jana azma ya serikali yake ya kutokomeza al-shabaab ndani ya mwaka mmoja.