Mwishoni mwa filamu “Titanic,” Rose anaelea juu ya kipande cha fremu ya mlango kilichopambwa kwa umaridadi huku mpenzi wake Jack aking’ang’ania ukingo wake, akimshika mkono.
Mashua ya uokoaji hatimaye inawasili, lakini baada ya muda ni kwa Rose tu, ambaye anaahidi “hatamwacha kamwe” Jack anapojiweka huru kutoka kwenye sehemu aliyoshika upande wa barafu naye anateleza chini ya Bahari ya Atlantiki na kuzama.
Sasa habari mpya ni kwamba kipande hicho cha mlango kimepigwa mnada na kuuzwa kwa mamilioni ya dola za Kimarekani.
Kipande hichi cha mlango kiliuzwa kwenye mnada kwa dola $718,750 zaidi ya Bilioni 1 za Kitanzania siku ya Jumamosi, sehemu ya kumbukumbu kutoka kwa Planet Hollywood.
Heritage Auctions ilisema katika taarifa kwamba hafla hiyo “ilivunja rekodi ya matarajio” na hata kuweka rekodi kwa minada ya kampuni ya vifaa vya sinema na mavazi, ikivutia zaidi ya wazabuni 5,500 kutoka kote ulimwenguni.