Katika kuendelea kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na vinakua salama Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu imeunda kamati Rasmi ya Kidakio cha Mto Ngerengere kinachohudumia wananchi zaidi ya milioni 3 wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Rasilimali za Maji zinalindwa na kuhifadhiwa,
Zoezi hili limefanyika katika makao makuu ya Ofisi ya Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu Iliyopo Mkoani Morogoro na kushirikisha Wadau mbalimbali Wakiwemo Jumuia za watumia maji,
Kupitia Jukwaa Hilo
Mkurugenzi wa Bodi ya maji Bonde la Wami/ Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy Ambae alikuwa Mgeni Rasmi amesema kamati hii itasaidia kutatua migogoro ya watumia maji na wadau wanaotegemea maji katika Kidakio cha Ngerengere na Kuhakikisha Mdau ananufaika na kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za kulinda Rasilimali za Maji katika eneo lake,
Kwa upande wa Mwanasheria kutoka Bodi ya maji Bonde la Wami/ Ruvu Bw. Aloyce Lyimo amesema kuwa undwaji wa kamati hiyo umefanyika kwa njia ya ushirikishwaji ambapo majina ya wajumbe yamependekezwa na Wadau waliohudhuria kwenye jukwaa na baadae kupelekwa kwenye Bodi na wajumbe kuanza kazi mara baada ya Kupendekezwa,
Aidha mwenyekiti wa kamati ya kidakio cha Ngerengere Bi. Pilly Kagosi amesema kuwa kwa nafasi yake aloyopewa atahakikisha
anasimamia zoezi hilo na kupata wajumbe hai ambao watakuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa Rasilimali maji,
Hata hivyo mmoja kati ya wadau nawaliohudhuria Ndugu Kobelo Kobelo ambaye ni Mwenyekiti wa jumuiya ya watumia Maji kidakio cha Ngerengere amesema kuwa amefurahishwa na zoezi hill kwa sababu nguvu itaongezeka katika usimamizi wa Rasilimali maji kwa
upande Ngerengere