Katika kuendelea kujenga mahusiano mazuri kati ya wafanyabishara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Mamlaka hiyo Mkoa wa Morogoro imekutana na wadau mbalimbali wa Kodi ikiwemo Madereva Bodaboda na bajaji.
Pamoja na Elimu iliyotolewa mamlaka hiyo imewataka wamiliki wa vyombo vya moto mkoani humo kuzingatia kubadilisha kadi za umiliki pindi wanapouza au kunua vyombo vya moto.
kauli hiyo imetolewa katika Kikao cha Madereva wa pikipiki za kubeba abiria pamoja na bajaji kilichoandaliwa na TRA Mkoa wa Morogoro na kushirikisha LATRA polisi pamoja na shirika la Bima.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Morogoro Chacha Gotora amewataka madereva hao kuzingatia sheria za mamlaka hiyo katika usajili wa vyombo vya moto.
Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea ikiwemo masuala ya kiusalama pamoja na mlundikano wa Kodi.
Nao baadhi ya madereva walipongeza TRA kwa elimu hiyo huku wakiomba kupunguziwa baadhi ya tozo.