KATIKA Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Wadau Mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam, Taasisi ya Huduma za Afya za Kiwango cha juu na Wadau wengine Wamekutana Kutambua Mabadiliko ya Tabianchi kama Tishio Kubwa la Afya ya Mwanamke Duniani kama ilivyotambuliwa na Shirika la Afya -WHO.
Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa The Choice Maria Matui ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Muungano wa Tanzania wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi (GCCTC), amepongeza Juhudi za Kutambua Mahitaji ya Kijamii ya Afya hasa kwa Wanawake, akizitambua Juhudi hizo Kama sehemu Muhimu ya Kutoa Huduma Bora kwa Wagonjwa kwa Kuzingatia Mahitaji.
Aidha amesema Wananchi wengi bado hawafahamu Kuhusu Madhara ya Moja Kwa Moja ya Mabadiliko ya tabia nchi hasa Waishio Vijijini lakini hali hiyo haimaanishi Kwamba Ufahamu wao si Sawa na ule ambao Sayansi inatambua ama Maandiko Mbalimbali ya Kitafiti yanachambua.
Kwa Upande wake Kiongozi wa Mradi wa Choice Kutoka Hospitali ya Aga Khan Profesa Ahmed Jusabani amesema Malengo ya Mradi huo ni Kutekeleza Vipengele Vitatu vya Dira ya Maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na Afya, Usawa wa Kijinsia na Mazingira huku akitaja Vita ya Urusi na Ukraine na COVID-19 kama Changamoto zilizokwamisha Kutekelezwa Mapema kwa Mradi huo.
Mradi wa Choice unatekelezwa Katika nchi Mbalimbali Duniani ikiwemo Pakistan, Kirgystan, Ghana, Kenya na Tanzania huku Ukilenga Kuikomboa Afya ya Mwanamke na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Mazingira.
Rachel