Bunge la Israel seneti Jumatatu lilipitisha sheria kuruhusu kufungwa kwa televisheni ya Al Jazeera ambapo sheria hiyo ilipitishwa kwa kura 71 hadi 10 katika usomaji wake wa pili na wa tatu katika bunge la Knesset.
Kusomwa kwa kwanza kwa mswada huo kulipitishwa Februari 12.
Chini ya mswada huo, waziri wa mawasiliano atapewa mamlaka ya kuzima mitandao ya kigeni inayofanya kazi nchini Israel na kuwanyang’anya vifaa vyao iwapo waziri wa ulinzi atabainisha kuwa matangazo yao yanaleta “athari halisi kwa usalama wa taifa.”
Kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo, Waziri wa Mawasiliano wa Israel Shlomo Karhi aliapa kwamba chaneli ya Al Jazeera inayofadhiliwa na Qatar itafungwa “katika siku zijazo.”
Mapema Jumatatu, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliapa “kuchukua hatua mara moja kufunga Al Jazeera” kufuatia kupitishwa kwa mswada huo katika Knesset.