Watafiti wanasema kuwa wameweza kutafsiri maana ya ishara za mawasiliano zinazotumiwa na Sokwe wanaoishi msituni
Watafiti hao wanasema, Sokwe hao huwasiliana kwa kutumia ujumbe 19 na kwa ishara 66.
Wanasayansi hao waligundua hili kwa kuwafuatilia na kuwanasa kwa video Sokwe nchini Uganda na kutathmini zaidi ya visa 5000 vya umuhimu wa mawasiliano hayo.
Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la Bayolojia ya kisasa.
Daktari, Catherine Hobaiter, aliyeongoza utafiti huo, anasema kuwa huu ndio mfumo pekee wa kimataifa wa mawasiliano kuhusu wanyama kuwahi kurekodiwa.
Ni binadamu pekee na Sokwe ambao wana mfumo wa mawasiliano ambapo walitumiana ujumbe kwa lengo fulani
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB