Taharuki imetokea katika Mtaa wa 14 kambarage uliopo Mjini Geita Baada ya Nyumba Moja katika Mtaa huo kuungua Moto huku chanzo chake kikidaiwa na Familia hiyo kusababishwa na Jiko la Gesi lililokuwa limewashwa na Dada wa kazi na Kupelekea kulipuka huku Baadhi ya Vitu vya Samani katika Nyumba hiyo vikiungua Moto.
Akizungumza kwa Niaba ya Familia Kaka aliyefahamika kwa Jina la Lucas Jeremiah mkazi wa Mtaa huo amedai kuwa alipata taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa Kaka ake ambaye ndiye Mmiliki wa Nyumba hiyo akimwambia kuwahi nyumbani kwake kwa ajili ya kwenda kuuzima moto huo huku akisaidiana na Majirani.
“Nilipofika haya Mazingira nilikuta moto una waka wananzengo wameshafungua visima kuchota maji wanamwaga ili kuzima ule moto uliokuwa unawaka vimeungua vyumba kama vitatu hivi uharibifu uliofanyika lakini cha msingi tuu ni kwamba ni ule usalama wa watu wangu Mwenye Familia na mtoto wake wote wako salama , ” Msemaji wa Familia Lucas.
Mmoja wa Majilani walioshuhudia tukio hilo Bi.Leah Kengele Pamoja na Balozi wa Mtaa 14 kambarage Ndg. Stephano Matata wamesema majira ya Saa tatu za Ahsubuhi wamepokea taarifa za kuungua kwa Nyumba ya Jirani huyo ambayo wanadai chanzo chake ni jiko la Gesi baada ya kufika katika eneo hilo wamejionea hali halisi ambapo Baadhi ya vitu kwenye nyumba vimeteketea kwa moto ikiwemo Vitanda , Magodolo pamoja na Nguo za watoto.
Akithibitisha kutokea kwa Tukio hilo Afisa Habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Geita ,Bahati Kamgisha amesema ni kweli tukio hilo limetokea na kudai kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la zimamoto na uokojai .