Kamishna wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA) Yusuph Juma Mwenda amesema mamlaka ya mapato imevuka lengo na kueka rekodi ya kila mwezi ndani miezi yote tisa ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kufanikiwa kwa ukuaji wa asilimia 104.34 kwa kukusanya Billioni 559.485
Mamlaka ya mapato Zanzibar kwa kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2023/2024 cha Julali ,2023-machi 2024 mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA) imefanikiwa kukusanya Jumla ya Tsh.559.485 Billioni kati ya lengo la kukusanya Jumla ya Tsh. 536.209 Billioni ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 104.34 ya lengo la makusanyo ya kodi tarajiwa
miezi tisa ya mwaka wa Fedha wa 2023/2024, Makusanyo halisi ya kodi yameongezeka kwa asilimia 24.53, ambacho ni kiasi cha Tshs. 110.202 Billoni,ukilinganisha na mapato halisi ya miezi tisa ya mwaka wa Fedha uliopita wa 2022/2023 ambayo yalikuwa ni Tshs. 449.283 Billoni. Sambamba na hilo, kwa mara ya kwanza, ZRA