Mbelgiji Marc Brys ameteuliwa kuchukua nafasi ya Rigobert Song kama kocha wa timu ya taifa ya Cameroon, wizara ya michezo ya nchi hiyo ilitangaza Jumanne.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 amefundisha klabu 15 katika maisha yake ya soka nchini Ubelgiji, Uholanzi na Saudi Arabia huku kazi yake ya mwisho ilikuwa miaka mitatu na Leuven.
Kocha msaidizi wa Brys atakuwa fowadi wa zamani wa Cameroon Francois Omam-Biyik, ambaye alifunga mabao 26 ya kimataifa kati ya 1985 na 1998.
Anachukua timu ambayo ilitupwa nje ya Kombe la Mataifa ya Afrika hivi majuzi na Nigeria katika hatua ya 16 bora.
Cameroon kwa sasa wako kileleni mwa Kundi D la Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026, kufuatia ushindi dhidi ya Mauritius na kutoka sare ya ugenini na Libya.
Mkataba wa Song haukuongezwa tena na rais wa shirikisho la kandanda la Cameroon Samuel Eto’o baada ya kuondoka kwa AFCON.