Kurejea kwa Neymar katika klabu ya Santos ya Brazil “kutafanyika hivi karibuni ” kulingana na baba na wakala wa mchezaji huyo, Neymar da Silva Santos Sr.
Fowadi huyo wa Brazil, ambaye anauguza jeraha la goti, alikuwa kwenye viti akitazama klabu yake ya zamani katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Palmeiras Jumapili.
Uvumi umeongezeka katika miezi ya hivi karibuni kwamba Neymar anaweza kurejea Santos mara tu mkataba wake na klabu ya Al Hilal ya Saudia utakapomalizika Juni 2025.
“Ndoto ni muhimu sana,” Neymar da Silva Santos Sr. aliambia TNT Sports. “Lakini nadhani tunahitaji kuwa watulivu kuhusu hili.
“Neymar bado ana muda wa kukaa nje ya Brazil, hasa Saudi Arabia. Hili [kurudi] litatokea wakati fulani. Lakini tunapaswa kuwa watulivu. Kwanza fikiria kuhusu kupona kwake, ambayo inahitaji kuwa nzuri, bora ili kuweza kurudi kwa kiwango cha juu.
“Kila mtu anajua mapenzi tuliyo nayo kwa Santos FC. Hapo ndipo maisha ya mwanangu yalipoanzia.”
Akiwa bidhaa ya vijana wa Santos, Neymar aliondoka klabuni hapo Juni 2013 na kujiunga na Barcelona.