Kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips atalazimika kukatwa mshahara mkubwa ikiwa anataka kurejea Leeds United, kulingana na Daily Star.
Huku West Ham wakiamua kutoubadilisha mkataba wa mkopo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuwa wa kudumu, Manchester City itatafuta mtu mpya.
City wangeachana na Phillips kwa pauni milioni 25, hata hivyo mshahara wake wa pauni 150,000 kwa wiki italazimika kupunguzwa sana ikiwa atarejea Leeds.
Leeds watavutiwa iwapo watapata nafasi ya kupanda tena Ligi Kuu wakati huohuo, Newcastle United pia wanaonyesha nia, huku Magpies wakiripotiwa kuwa wanaweza kufikia mshahara wake.