AFISA TATIBU AKUTWA AMEFARIKI DUNIA CHUMBANI KWAKE GEITA.
Afisa Tabibu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Geita anayefahamika kwa Jina la Fimbo Ncheye amefariki dunia kwa kujiua akiwa ndani ya chumba alichokuwa amelala huku akiacha ujumbe wa kuwaomba radhi wazazi wake kwa hatua aliyoichukua na kutaka mtu yeyote asilaumiwe juu ya kkifo chake .
Akizungumzia tukio hilo Mmiliki wa nyumba aliyofia Cheye Mwiseo amesema usiku wa kuamkia leo Majira ya saa tano aligongewa na wapangaji wakidai wanasikia kelele za fujo kama mtu anaugulia na kuomba msaada lakini walipofika walikuta kelele zimetulia na walipogonga hakufungua mlango.
“Nilipofika nilikuta kelele zimetulia nikawauliza alikua amekunywa pombe wakadai hawakumuona alivyoingia na wamegundua kelele tulipoona hafungui tuliamua kumpigia simu aliyepanga chumba maana huyu alikua amekuja kumshikia tuu mwenzake aliyesafiri, kumekucha asubuhi hatujaona akitoka tumeenda kwa viongozi na polisi walipokuja ndio wakavunja mlango na kumkuta amekufa na mezani kulikua na dawa , ” Proces Mwiseo.
Akithibitisha kutokea kwa Kifo hicho Mganga Mfawidhi katika Hospitali hiyo Thomas Mafuru amesema Afisa Tabibu huyo alikuwa akijitolea katika kitengo cha wagonjwa wa Nje OPD na hakua Mgonjwa na hakuwai kueleza kama alikuwa na tatizo lolote.
” Imetokea tuu ghafla tumepigiwa simu na kuambiwa mwenzetu amefariki kwenye chumba nah ii ni kesi ya polisi naomba nisieleze sababu za kifo na hadi anaondoka kazini jana alikua vizuri hakua na shida yoyote ametibu wagonjwa bila shida yani hii imetokea tuu ghafla ,” Dkt. Mafulu.
Dk Mafuru amesema hadi sasa hawajafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo na kwamba wanasubiri taratibu za kipolisi pamoja na familia ili mwili wake kufanyiwa uchunguzi.
Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Adam Maro alipotafutwa na Millard ayo kwa njia ya simu amesema yupo kwenye ofisi nyingine na kuomba kupewa muda ili aweze kufuatilia tukio hilo.