Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa tangu kuchaguliwa kwake kama rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye alisema moja ya hatua zake za kwanza za sera itakuwa kukagua sekta ya mafuta, gesi na madini ili kung’oa rushwa.
“Unyonyaji wa maliasili zetu, ambazo kwa mujibu wa katiba ni mali ya wananchi, utapokea kipaumbele maalum kutoka kwa serikali yangu,” alisema Faye katika hotuba ya jadi ya rais aliyoitoa siku moja kabla ya siku ya uhuru wa nchi.
“Nitaendelea na ufichuzi wa umiliki bora wa makampuni ya uziduaji [na] na ukaguzi wa sekta ya madini, mafuta na gesi.”
Maendeleo ya kwanza ya mafuta katika pwani ya Senegal yanatarajiwa kuanza uzalishaji katikati mwaka huu.
Mradi wa mafuta na gesi wa Sangomar, unaoendeshwa na Kampuni ya Australia ya Woodside Energy, unatarajiwa kuzalisha takriban mapipa 100,000 kwa siku.