Upinzani wa Togo siku ya Alhamisi uliitisha maandamano makubwa ya siku tatu kupinga uamuzi wa serikali kuchelewesha uchaguzi wa wabunge wa mwezi huu.
Mvutano kati ya serikali ya Rais Faure Gnassingbe na upinzani umeongezeka kufuatia bunge kuidhinisha wakosoaji wa mabadiliko ya katiba wanaopingwa wanasema ni jitihada za kumbakisha kiongozi wa Togo madarakani.
Ofisi ya rais ilitangaza Jumatano kwamba mashauriano zaidi yanahitajika kuhusu mageuzi hayo na kusimamisha uchaguzi wa wabunge na wa kikanda wa Aprili 20 bila kutoa tarehe mpya.
Vyama vinne vya upinzani na jumuiya ya kiraia vilitoa tamko la kutaka maandamano yafanyike Aprili 11, 12 na 13.
“Watia saini wanalaani vikali ujanja wa serikali, ambao unajaribu kwa kila njia kuidhinisha mapinduzi yake ya kikatiba,” taarifa ya upinzani ilisema.
Mzozo huo wa mageuzi umechochea mjadala kuhusu utawala wa Gnassingbe, ambaye amekuwa madarakani tangu 2005 baada ya kumrithi babake, ambaye alitawala kwa miongo mitatu baada ya mapinduzi ya kijeshi.