Israel itaruhusu uwasilishaji wa “muda” wa misaada kupitia mpaka wake na Ukanda wa kaskazini wa Gaza, ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilitangaza siku ya Ijumaa.
Taarifa ya serikali ilitolewa saa chache baada ya onyo kutoka kwa Rais wa Marekani Joe Biden.
Biden aliionya Israel kuhusu mabadiliko makali katika sera yake kuhusu vita vya Gaza Alhamisi huku kukiwa na hali ya sintofahamu katia ya marekani na utawala wa Benjamin Netanyahu na shinikizo la ndani linaloongezeka katika mwaka wa uchaguzi wa Marekani.
Biden amesimama kidete nyuma ya Israel tangu mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7, na ukosoaji wake wa vifo vya raia huko Gaza haujazuia Washington kusambaza vifaa vya kijeshi kwa mshirika wake muhimu.
Katika mazungumzo ya muda wa dakika 30 na Netanyahu baada ya mashambulizi ya Israel kuwaua wafanyakazi saba wa misaada huko Gaza kutoka shirika la misaada lenye makao yake makuu nchini Marekani la World Central Kitchen, Biden kwa mara ya kwanza, Biden “aliweka wazi kwamba sera ya Marekani kuhusu Gaza itaamuliwa na tathmini yake ya hatua ya haraka ya Israel” kukomesha mauaji na hali mbaya ya kibinadamu, White House ilisema.