Klabu ya Saudi Pro League Al Nassr inatazamia kumnasa Fernando Hierro kwenye klabu yao, kwa mujibu wa Record.
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania, Hierro amekuwa mkurugenzi wa michezo katika Klabu ya Deportivo Guadalajara ya Mexico tangu Oktoba 2022 akiwa ameshikilia wadhifa huo hapo awali katika FA ya Uhispania.
Al Nassr wanatafuta mkurugenzi wa michezo na wamempa Hierro kipaumbele chao baada ya mazungumzo na mtendaji mkuu wa Ureno Miguel Rubero kuvunjika.
Tazama pia…