Mgombea Urais wa chama cha Republican Donald Trump, kwa mara nyingine tena Jumamosi (Aprili 6) alisisitiza matamshi yake dhidi ya wahamiaji kutoka Afrika, Asia na Mashariki ya Kati, na kulaumu kwamba watu kutoka nchi “nzuri” “kama Uswizi” hawakuwa wakihamia Marekani.
Akizungumza katika harambee ya mamilioni ya pesa katika jumba la kifahari linalomilikiwa na bilionea mfadhili John Paulson huko Palm Beach, Florida, Trump mhudhuriaji katika uchangishaji fedha, alizungumza kwa kina kuhusu wahamiaji wanaoingia Marekani.
Akilaumu Biden kwa wahamiaji haramu, Trump alisema: “Hawa ni watu wanaoingia kutoka magereza ,wanatoka katika maeneo na nchi zisizoaminika, nchi ambazo ni janga.”
Akionekana kurejelea kauli yenye utata ambapo aliielezea Haiti na baadhi ya mataifa barani Afrika kama “nchi yenye janga”, alisema, “Na niliposema, unajua, kwa nini haturuhusu watu kuingia kutoka nchi nzuri, Ninajaribu kuwa mzuri.”
“Nchi nzuri, unajua, kama Denmark, Uswizi? Je, tuna watu wowote wanaokuja kutoka Denmark? Vipi kuhusu Uswisi? Vipi kuhusu Norway?”
“Na unajua, walichukua hiyo kama maoni mabaya sana, lakini kwangu ni sawa,” aliongeza.