Papa Francis Jumapili aliwataka viongozi wa kisiasa kusimama na kufanya juhudi za kupatanisha na kujadili njia ya amani katika Mashariki ya Kati na Ukraine.
Akizungumza wakati wa hotuba ya Regina Coeli, papa aliwaalika waumini kutokosa kuendelea kuombea amani.
“Amani ya haki na ya kudumu, haswa kwa Ukraine inayoteswa na Palestina na Israeli,” alisema.
“Roho wa Bwana Mfufuka awaangazie na kuwaidhinisha wale wote wanaofanya kazi kupunguza mvutano, na kuhimiza ishara zinazowezesha mazungumzo,” aliongeza.
Papa ametoa wito mara kwa mara kutaka mizozo hiyo miwili ikome, akiwataka viongozi kufanya mazungumzo ili kumaliza ghasia hizo.
Siku ya Jumatano, papa alitoa wito upya “kwa raia waliochoka na wanaoteseka waruhusiwe kupata misaada ya kibinadamu na mateka waachiliwe mara moja.”