Jumapili iliadhimishwa miezi sita tangu Hamas ilipoanzisha mashambulizi ya kushtukiza ya kigaidi kusini mwa Israel na Israel ilijibu kwa kutangaza vita dhidi ya Hamas.
Israel ilifanya mashambulizi ya ardhini mwishoni mwa mwezi Oktoba, ikiimarisha vikwazo vyake vya usafirishaji wa bidhaa na watu kutoka Gaza na kuwaamuru raia wa kaskazini kuhama kuelekea kusini.
Katika muda wa siku 182 zilizopita, Israel ikitekeleza lengo lake la kuiangamiza Hamas, hali mbaya ya kibinadamu imetokea huko Gaza, huku kukiwa na uhaba wa chakula, maji safi na dawa, pamoja na kuporomoka kwa mfumo wa huduma za afya.
Tangu shambulio la kushtukiza la kigaidi la Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023, idadi ya vifo katika pande zote mbili za mzozo imekuwa ikiongezeka kwa kasi.
Nchini Israel, takriban watu 1,700 wameuawa na wengine 8,700 kujeruhiwa, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel. Idadi ya waliouawa ni pamoja na zaidi ya raia 800, takriban wanajeshi 600 wa IDF na polisi 61.