Wahamiaji haramu 17 raia wa Ethiopia wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na Kibali huku zikiwa zimepita siku 14 pekee toka kukamatwa kwa wahamiaji wengine haramu 20 raia wa Ethiopia.
Akiongea na Ayo Tv Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara Acp Lukas Mwakatundu amesema Wahamiaji hao wamekamatwa Jana April 7 Baada ya dereva wa gari hilo kugoma kusimamishwa na Polisi katika kizuizi cha Minjingu na baadae Polisi kumfuatulia ndipo Dereva kutelekeza gari hilo na kutokomea vichakani.
Tukio hili limetokea zikiwa zimepita siku 14 Toka kwa kukamatwa kwa wahamiaji haramu wengine 20 raia wa Ethiopia katika kizuizi cha Minjingu wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruze V8 ambayo ilikutwa na Bendera ya CCM,
“Jana tarehe 7 katika kizuizi cha Minjingu Kuna gari lilitupita pale likagoma kusimama likagonga kizuizi ndipo Polisi wakapata wasiwasi kwamba kwanini amegoma kusimama ndipo tukaanza kumfuatulia mpaka eneo la Kiongozi ndipo Dereva wa gari hili akashuka na kutelekeza gari likiwa na Wahamiaji hao haramu 17 wote kutoka Ethiopia,gari hili lililokamatwa ni Land Cruze V8 ambayo lilikuwa na namba za bandi za Serikali lakini namba zake halisi ni T723 BSF na Sasa gari hilo lipo Polisi”
“Gari hili na Plate namba zake havihusiani na Mali ya Serikali maana ata kwenye Usajili wa gari hili unaonyesha ni Mali ya mtu binafsi na uchunguzi unaendelea” ACP Mwakatundu