Jeshi la polisi mkoani Mbeya limesema watoto watatu wa familia moja wakazi wa kitongoji cha Gengeni kata ya Kambikatoto wilaya ya Chunya mkoani humo wamefariki baada ya kuvamiwa na kuliwa na fisi usiku wakiwa wamelala nyumbani kwao huku Wazazi wao nao wakijeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya, Abdi Issango amesema tukio hilo limetokea April 7, 2024 usiku ambapo Fisi huyo alivamia nyumba ya Shigela Ngasa (45) Mkazi wa Gengeni na kuwaua kwa kuwang’ata Watoto hao ambao ni Samweli Shigela (5) Kasunzu Shigela (3) na Ngasa Shigela (1) wote Wakazi wa Gengeni na kuwajeruhi Wazazi ambao ni Shigela Ngasa na Mke wake Limi Masanja (38) ambao kwa sasa wamelazwa Hospitali.
“Polisi kwa kushirikiana na Askari wa wanyamapori kutoka pori la akiba la Rungwa na Wananchi wa Gengeni wamefanikiwa kumuua fisi huyo ambaye alikimbilia porini na baadae kurudi tena Kijijini hapo kisha kuuawa” Kamanda Issango.