Mwananchi aliyefahamika kwa Majina ya Dotto Bunuma Mkazi wa kata ya Kanyala Halmashauri ya Mji Geita Amemshitakia ndugu Michael Mkomwe Mkazi wa kata hiyo kwa tuhuma za kuchukua eneo la Baba yake lenye thamani ya shilingi Milioni mbili kwa madai ya kuwa Baba yao alimuuzia kipindi yeye akiwa Masomoni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa wilaya uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya kusikiliza kero uliofanyika kata ya Kasamwa Mlalamikaji Ndugu Dotto Bunumwa amesema baada ya kupata taarifa ya upimaji viwanja alirudi nyumbani na kukuta eneo hilo tayari limejengwa nyumba na Mtu ambaye si mwanafamilia na Baadae aliwasilisha katika ofisi za Serikali ya Mtaa nakuambiwa eneo hilo limekwisha kuuzwa na Baba ake mzazi jambo ambalo halina ukweli ndani yake.
Ameendelea kusema baada ya kuona hiyo hali aliomba wakubaliane rasmi kuuziana eneo hilo lakini baada ya kuitwa katika ofisi za Mtaa huo Mnunuzi kwa ajili ya kukubaliana alimtolea maneno yenye lugha chafu ya kutaka kumdhohofisha ndipo Dotto alichukua uwamzi wa kufungua kesi katika ofisi hiyo lakini bado alionekana eneo hilo limeuzwa na Baba yake licha ya Mzazi wake kuwa na Changamoto ya Kuona (Kipofu).
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Kanyala amesema baada ya kupata vielelezo kutoka Ofisi ya Mtaa na kujilidhisha alibaini tayari kulikuwepo na Makubaliano baina ya Baba mzazi wa Dotto Bunumwa na Mnunuzi Michael Mkomwa ndipo waliamua eneo hilo kumilikishwa kwa Mnunuzi .
Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashimu Komba baada ya kupata malalamiko kwa upande wa Mlalamikaji ameunda timu ya watu watatu ikiongozwa na Mwanasheria wa Halmashauri ambao wataenda kujilidhisha katika kukagua nyaraka hizo pamoja na kusikiliza Upande wa Mlalamikiwa ambaye hakuwepo katika mkutano huo na walete majibu pamoja na kutatua Mgogoro huo.