Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Ruangwa, Aprili 08,2024 imemhukumu Mussa Saidi Arife (34), mkazi wa kijiji cha Mbekenyera wilaya ya Ruangwa, kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kuvunja jengo na kuiba.
Hukumu hiyo ya kesi namba 20 ya mwaka 2023 imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Yasinta Kingwala.
Awali mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 12,2023 huko kijiji cha Mbekenyera baada ya kuvunja duka la Fatuma Said Kaepe na kuiba vitu vyenye thamani ya shilingi 750,000/=.
Upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na mwendesha mashitaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Rashidi Nalleche ulileta mashahidi sita ambao walitoa ushahidi wao wa kuthibitisha tukio hilo, ushahidi ambao mahakama hiyo iliridhika nao na kumuona mtuhumiwa anayo hatia.