Waraibu wa dawa za kulevya huko Sierra Leone, Afrika Magharibi, wanachimba makaburi ili kutumia dawa wanayoiita ‘Zombie’ iliyotengenezwa kwa kutumia mifupa ya binadamu iliyoharibika kiasi hali hii imepelekea serikali kutangaza hali ya hatari ya kitaifa ili kukabiliana na tishio hilo.
Mamlaka sasa inalinda makaburi ili kuzuia zoezi la uchimbaji wa mifupa kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za ‘Zombie’.
Dawa hiyo, iliyopewa jina la ‘kush’, ina mfupa wa binadamu uliosagwa kama mojawapo ya viambato vyake kuu.
Dawa hiyo ya mihadarati ilionekana kwa mara ya kwanza nchini Sierra Leone mwaka wa 2018.
Matumizi mabaya ya dawa za kulevya ya dutu hii ya kiakili imeongezeka na kuwa changamoto ambayo haijawahi kushuhudiwa kwenye serikali ya mtaa.
Wafanyabiashara sasa wanageuka kuwa wezi wa makaburini, kuvunja maelfu ya makaburi ili kuiba mifupa ili kuendana na mahitaji yao.
“Nchi yetu kwa sasa inakabiliwa na tishio lililopo kutokana na athari mbaya za dawa za kulevya na utumiaji mbaya wa dawa za kulevya, haswa dawa mbaya ya sintetiki Kush,” Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio alisema, kulingana na BBC.
Bio, pamoja na kukiri “kuongezeka kwa vifo” kati ya watumiaji wa dawa za kulevya, pia alisema kuwa ameunda kikosi kazi cha kutokomeza tishio la dawa za kulevya.
Sierra Leone sasa inajenga vituo katika kila wilaya “vina wahudumu wa kutosha na wataalamu waliofunzwa kutoa huduma na usaidizi kwa watu walio na uraibu wa dawa za kulevya”.