Mbunge Wa jimbo la Monduli Fredrick Lowassa ameendelea na ziara yake katika jimbo hilo kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo , ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kusikiliza na kutatua Kero Mbalimbali za Wananchi katika Kata ya Selela .
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo jipya la Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Oltinga, Wakati akisomewa taarifa ya jengo hilo Changamoto kubwa iliyoonekana ni uhitaji wa vitanda 104 Ambapo mbunge huyo alikubali kuichukua kama changamoto na kuahidi kufanyia kazi kwa wakati mfupi ili wanafunzi wapate pa kulala.
“Tumefika hapa tumetembea na tumezungumza na wanafunzi, Risala ikasomwa lakini kwa msisitizo zaidi ilikuwa ni changamoto la Bweni letu ambalo lilikuwa halina vitanda , kitu ambacho tunapaswa wote kujua Shule ya Oltinga ilianzishwa mwaka 2007, Shule ya Oltinga ni mmoja kati ya waasisi wa Shule za kata nchi nzima , Wakati mzee Lowassa anataka kuanzisha shule za kata nchi nzima alisema lazima kwanza aaanze na jimbo lake , kwa hiyo nilipofika pale nikasema pamoja na Changamoto zingine na mimi nataka niache Alama katika Shule hii ya Oltinga kwa kutoa vile vitanda 104 kulingana uhitaji wa Mwalimu mkuu katika taarifa yake” Amesema Fredrick
“Tumetoka hapo tukaenda kwenye tank kubwa hili hapa Ambalo linatoa maji lositeti, Ni Tank nimekaa na viongozi Nathani nimeambiwa Tank lile lilijengwa Mwaka 1951, lilijengwa na wajerumani kwa Ajili ya kusaidia mifugo kupata maji Wakati ule , Mwaka 51 hata mzee Lowassa hakuzaliwa hahhahahaha, lakini lazima tukubali technologia ya wenzetu pamoja na changamoto ndogondogo la Tank lile bado linaonekana lina uimamara sana , Nguvu za Wananchi ni kubwa kujenga Eneo la Mifugo kunywa Maji na Ripoti nimeona hongereni sana na kwa changamoto zilizobakia nimechukua ili kuzifanyia kazi” Amesema Fredrick