Manchester City wanaongoza mbio za kumnasa kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Jamal Musiala, linaripoti Independent.
Kikosi cha Pep Guardiola ni mojawapo ya vilabu vinavyomfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ingawa nia yao iko katika hatua ya juu zaidi kuliko wapinzani, huku Liverpool, Barcelona na Paris Saint-Germain pia wakimtaka.
Musiala ni mmoja wa wachezaji wawili muhimu ambao City wanataka kuwafanya majira ya joto ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji na anaweza kuwa tayari kuondoka Allianz Arena, ambako anatafuta uhakika kwamba timu hiyo ya Bundesliga itaweza kushindana katika kiwango cha juu.
Amesalia kuwa mchezaji muhimu kwa meneja Thomas Tuchel msimu huu, amechangia mabao 16 katika mechi 23 za ligi, lakini ataingia miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake msimu wa joto, na mkataba wake unakamilika msimu wa joto wa 2026.