Kiwanda hiki cha kwanza cha biashara duniani cha kugeuza kinyesi cha binadamu kuwa nishati endelevu ya anga (SAF) kimetangazwa huuku kampuni hiyo ya nishati ya mimea Firefly ikipanga kuendeleza kiwanda hicho huko Harwich, Essex, na inatarajia kusambaza mafuta kufikia 2028.
Imefikia makubaliano na Wizz Air kutoa hadi tani 525,000 za mafuta hayo katika kipindi cha miaka 15.
Mtendaji mkuu wa Firefly James Hygate alisema biosolidi ni “aina ya vitu vya kuchukiza” lakini ina “rasilimali ya kushangaza”.”Tunageuza maji taka kuwa mafuta ya ndege.
Siwezi kufikiria mambo mengi ambayo ni mazuri kuliko hayo,” Bw Hygate aliongeza.
Uzalishaji wa mafuta hayo unahusisha kutumia takriban 70% chini ya kaboni kuliko mafuta ya kawaida ya ndege, lakini ni ghali mara kadhaa zaidi kuzalisha.
Kuna njia mbalimbali za kutengeneza SAF lakini nyingi ni ghali zaidi kuliko mafuta ya kawaida ya ndege ya taa, na usambazaji mdogo wa malisho ya taka kama vile mafuta ya kupikia yaliyotumika.
Afisa mkuu wa operesheni wa Firefly, Paul Hilditch, alisema maji taka yaliyobadilishwa yanapaswa kuwa ya bei nafuu na mengi zaidi, kutoa hadi 5% ya mahitaji ya mafuta ya mashirika ya ndege nchini Uingereza.