Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amewataka wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi ili kujikinga na mafurikio ya mvua za vuli zinazoendelea kunyesha.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea na kujionea maeneo yaliyokubwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya ya Mlimba mkoani Morogroro jana ambapo amewaomba wananchi kuendelea kufuatilia na kusikiliza ushauri wa serikali.
“Niwaombe wananchi tuendelee kushikamana ili kupambana na majanga ya Mvua na Mafuriko, ambayo yameleta kadhia kubwa sana kwa wananchi.
Serikali imetengeneza Mpango wa Dharura wa kukabiliana na mvua za El Nino na mvua za Masika, ambapo serikali itafanya kila linalowezekana kuzuia madhara yasitokee na hasa maisha ya watanzania,” alisema Waziri Mhagama