Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila ameongea na waandishi wa habari Ofisini kwake leo kuhusiana na bomoabomoa ambayo inaendelea eneo la Msimbazi
“Kuna bomoabomoa inaendelea pemebezoni mwa Mto Msimbazi ukianzia Jangwani zitabomolewa nyumba nyingi na nyumba hizi ni naada ya Wakazi wengi kulipwa fidia, tayari tumeshalipa fedhq zaidi ya Bilioni 50, wananchi wanapisha mradi mkubwa wa uboreshaji wa kingo za Mto Msimbazi, ujenzi wa miundombinu ya kisasa” RC Chalamila
“Wale wote ambao mmeshalipwa fidia msiende tena kujenga kwenye maeneo ya mabonde ambapo kesho mtavamiwa na maji na mwisho wa siku kuwa karaha na sio raha, tumieni fedhq mlizopata kujenga kwenye maeneo mazuri, ambayo hayana migogoro”
“DSM ni kweli kwamba barabara nyingi zimrharibika, niwaombe Watanzania tuendelee kuwa na usikivu wakati huu wa mvua nyingi” RC Chalamila
“Tunajipanga ili tuweze kuingiza magreda soon mara baada ya mvua hizi kupungua, lakini jambo zuri muda sio mrefu, barabara zifuatazo zitatangazwa ili ziweze kupata wajenzi, Jimbo la Ilala peke yake barabara zipatazo Kilimita 20.9 zitaanza kujenga” RC Chalamila
“Kariakoo itakua KM 7.8 , Upanga KM 4.6, Ila KM 8.5, Ukonga barabara kubwa ya Banana, Kivule, Kitunda, Msongola itajengwa kwa kiwango cha Lami kwa KM 12.97” RC Chalamila Akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake