Kundi la watu 22 linalojumuisha watetezi wa haki za binadamu na watunga sheria, wamewasilisha rufaa katika mahakama kuu kupinga sheria tata ya ushoga alioidhinishwa mwaka uliopita nchini Uganda.
Rufaa hii inawasilishwa baada ya mahakama ya katiba mapema mwezi huu kutupilia mabali kesi iliokuwa imewasilishwa na kundi hilo kupinga sheria hiyo.
Kupitia wakili wao, Nicholas Opiyo, kundi hilo limeelezea kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo, hususan uamuzi kwamba kuidhinishwa kwa sheria hiyo hakukuwa kinyume cha katiba ya nchi hiyo.
Sheria hiyo inapendekeza adhabu ya hadi kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana kwenye mahusdiano ya jinsia moja, pamoja na uwezekano wa makosa ya ushoga kuadhibiwa kifo.
Sheria hiyo pamoja na hatua ya mahakama ya katiba ya mapema mwezi huu, imekashifiwa vikali na mashirika ya haki za binadamu, zikiwemo nchi za magharibi kama Marekani.