Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK. Emmanuel Nchimbi, ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Baada ya kumaliza katika Mkoa wa Songwe, ziara hiyo yasiku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.