Filamu ya “The Royal Tour ambayo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameshiriki akiwa mshiriki/mwongozaji mkuu imekua na mafanikio makubwa sana katika kutangaza vivutio vya utalii na urithi wa sanaa na utamaduni wa nchi yetu, kwani kupitia filamu hiyo kumekua na ongezeko kubwa la idadi ya watalii nchini ikilinganishwa na kipindi kabla ya kuzinduliwa kwa filamu hiyo.
Haya yamebainika Bungeni wakati Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) akijibu swali la Mhe. Amina Daud Hassan (Mb) ambaye alitaka kujua idadi ya watalii waliongia nchini tangu kufanyika kwa filamu ya Royal Tour iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais ili kutangaza nchi yetu.
Aidha Mhe. Kitandula aliongeza kuwa tangu filamu hiyo izinduliwe idadi ya watalii imeongezeka ambapo kuanzia mwezi Mei hadi Disemba Mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la asilimia 40.38 la idadi ya watalii ambayo ilifikia 1,086,143 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa Mwaka 2021 ambapo idadi ya watalii ilikuwa 647,595.
Aidha, idadi ya watalii iliendelea kuongezeka kwa asilimia 16.6 hadi kufikia watalii 1,302,271 kutoka watalii 1,086,143 kwa kipindi cha Mei hadi Disemba 2023. Vilevile, kwa kipindi cha Januari hadi Disemba Mwaka 2023 idadi ya watalii pia imeendelea kuongezeka hadi kufikia watalii 1,808,205 ukilinganisha na watalii 1,454,920 waliotembelea nchi yetu kwa kipindi kama hicho Mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 24.3.
“Hivyo, ni dhahiri kuwa filamu ya Tanzania “the Royal Tour” imekuwa na matokeo mazuri sana katika sekta ya utalii na ni vema Watanzania wote kwa pamoja tukaunga mkono juhudi za Mhe. Rais” alisema Mhe. Kitandula.
Kwa upande Mwingine Mhe. Kitandula akijibu swali la Mhe. Kilumbe Shaban Ng’enda (Mb) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuweka vivutio vya utalii katika mji wa Ujiji ili watu mbalimbali duniani waweze kutembelea.