Klabu ya Yanga leo imetangaza kuingia Mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na Kampuni ya Silver General Investment ambapo Kampuni hiyo inajihusisha na utoaji wa mikopo ya simu na kulipa kidogo kidogo.
Taarifa hizo zimetolewa na Rais wa Yanga Hersi Said ambaye amesisitiza wana Yanga kuchangamkia fursa hiyo kwani ni kuisapoti pia timu yao.
“Mwanachama na Shabiki wa Young Africans ambaye anahitaji kukopeshwa simu anapaswa kutoa kiasi cha Tsh 75,000 na kiasi kinachobaki analipa kidogo kidogo. Ndani ya simu utapata App ya Yanga SC ambayo imelipiwa kwa miezi miwili na nusu. Natoa wito kwa Wanachama wa Young Africans SC kuikimbilia fursa hii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Klabu yako” – Hersi Said
“Wataalamu wetu wa Silver General Investment watatoa semina ya namna gani simu hizi za mkopo zinapatikana na zinapaswa kulipiwa. Kimsingi simu hizi hazitalipiwa kwa kutoa hela keshi. Watakuwa na mumo maalum wa kulipia ili kuepukana na matapeli ambao wanaweza kuathiri biashara hii. Tutatumia matawi yetu kuratibisha mfumo mzima wa ukopeshwaji
na ulipaji ili kudhibiti mwenendo mzima wa biashara hii” – Hersi Said