Mitambo ya kisasa ya kupima ujazo wa mafuta ya aina zote yanayoingia nchini Tanzania (Flow Meters) ambayo imesimikwa katika Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara inatajwa kuinufaisha Serikali pamoja na wadau wa sekta ya mafuta.
Mitambo hiyo iliyosimikwa kwa awamu tatu na Serikali chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ina lengo la kupata takwim sahihi za mafuta, yakiwemo ya kula, taa, ndege, petroli, dizeli, ya vilainishi na mafuta mazito mara yanaposhushwa kutoka kwenye meli.
Lengo la mitambo ni kuifanya teknolojia kuwa utashi, hivyo kupunguza makosa ya kibinadamu.
Mhandisi Malago ameyasema hayo wakati wa ushiriki wa kuhakiki wa mitambo hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema awali vilikuwa vinatumika vipimo visivyostahiki vya Dip Sticking na UTI.
“Hii mitambo mipya ina faida, kwanza Serikali inapata kodi na tozo stahiki zinazotokana na uingizaji wa mafuta nchini kutokana na utambuzi sahihi wa kiwango cha mafuta,” Malago.
Ametaja faida nyingine kuwa ni kuongezeka kwa shehena ya mafuta yanayogizwa na nchi za jirani kupitia Bandari ya Dar es Salaam ambazo zitalipwa kodi stahiki.