Gwiji wa Brazil Romario, 58, amejisajili kama mchezaji wa Klabu ya Soka ya Amerika huko Rio de Janeiro, ambako pia anahudumu kama rais wa klabu.
Baada ya usajili wake kuidhinishwa Jumanne, mshindi huyo wa Kombe la Dunia la 1994 anapatikana kuchezea klabu hiyo katika kitengo cha pili cha michuano ya Carioca ligi ya jimbo la Rio de Janeiro — itakayoanza Mei 18.
Shirikisho la soka la Rio de Janeiro lilithibitisha kusajiliwa kwa Romario kuwa mchezaji na kuongeza kuwa atapokea kima cha chini cha mshahara ambacho kitatolewa kwa klabu.
Romario hakuwa wazi ni lini ananuia kuichezea klabu hiyo. Alisema hatashiriki katika mechi yoyote ya ligi, lakini akasisitiza anataka kucheza pamoja na mwanawe, aliyesajiliwa hivi karibuni na Amerika FC, Romarinho, ambaye ni mshambuliaji.
Aliwahutubia mashabiki wa vilabu hivyo katika chapisho kwenye Instagram, akisema: “Sitashiriki michuano, lakini nicheze mechi chache kwa timu ya moyo wangu na kutimiza ndoto nyingine, kucheza pamoja na mwanangu. unafikiri?”
Romario alicheza mchezo wake rasmi wa mwisho mnamo Novemba 2009 alipoichezea America FC, klabu pendwa ya baba yake, Edevair.
Amehudumu kama rais wa Amerika FC tangu 2009. Miaka mitano baadaye, alichaguliwa seneta wa Rio de Janeiro.