Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuweka kipaumbele kupitia bajeti ya mwaka huu ikiwemo kujenga Skuli za kisasa za Maandalizi, Msingi , Sekondari , Vituo vya mafunzo ya amali na Dahalia.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Skuli ya ghorofa ya Msingi Hamid Ameir iliyopo Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe: 17 Aprili 2024 ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka Wizara ya Elimu kuendeleza mpango wa kuajiri walimu wa kutosha wa Skuli zote na kuboresha maslahi yao.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa kila mzazi kuhakikisha anapeleke watoto kusoma katika Skuli zinazojengwa.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Muungano wa Tanzania ni wa kipekee unaoimarika tangu mwaka 1964 hadi leo na una faida nyingi.